//
Ads

Kubenea apigiria msumari Mwigulu kujiuzuru


MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, Saed Kubenea ameunga mkono wito wa wanafunzi, Asasi za kiraia, vyama vya kihiari, Mashirika ya Dini na watu wote wanaoipenda Tanzania wanaomtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ya nchi awajibike kwa kujiuzulu kutokana na kifo kilichotokea cha Akwilina Akwilini.

Hakuna shaka kwamba kifo cha Akwilina kimetokana na Risasi iliyorushwa na watu wanaomiliki silaha hasa Jeshi la Polisi.

Nimeona kwenye posti zake Mwigulu Nchemba kwenye group la Whatsapp linaitwa Siasa Vijana forum, Mh. Mwigulu alikuwa anajibu shinikizo la wanafunzi wakiongozwa na Abdul Nondo aliyekuwa anashinikiza Mwigulu ajiuzulu.

Tokea akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi amekuwa na winbo wa kuinyooshea kidole Chadema juu ya ugaidi hata kabla mimi sijawa Chadema, amekuwa anatembea na mtu mmoja aliyemwagiwa tindi kali kule Igunga na akiwatuhumu Chadema kwamba ndio walimwagia tindikali wakati taarifa zilizopo walimwagia tindikali wenyewe (inavyosemekana).

Kuna mlolongo mwingi, historia ndefu ya kumuhusisha Mwigulu Nchemba  na mambo machafu ambayo yametokea kwenye nchi hii na yeye akihusisha Chadema.

Mh Mwigulu anasema kwamba waliyempiga Risasi muuza magazeti wa Morogoro anaitwa ni Chadema na baadaye Chadema wakaisingizia Polisi, jambo hili limetokea zamani sana naamini wakati huo sikuwa Chadema lakini kwa kuweka rekodi sawasawa nikiwa Mwandishi wa habari za uchunguzi na uchambuzi.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Chadema wakati muuza magazeti huyo anapigwa na Wilbroad Peter Slaa, matukio ya kihalifu hayaweza kufanyika bila Mtendaji Mkuu wa chama kujua kama matukio yanafanywa na chama kwa sababu ni lazima hao watu walipwe na hakuna anaoweza kuwalipa kama sio Katibu Mkuu, kama Katibu Mkuu alikuwa Dk. Slaa na akawa anaongoza chama cha kigaidi leo ni Dk. Slaa ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden maana yake nini? Maana yake ni kwamba ama Mwigulu hajui kazi yake ama hizi ni porojo.

Kama yeye ni Waziri wa ndani na Rais amemteua Slaa kuwa Balozi na yeye bado anaendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na anajua Slaa na Chadema ni Magaidi yeye anafanya nini kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani?
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Unknown

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment